Wednesday, May 23, 2012

UREMBO/MATUMIZI YA POCHI.


Mwanamke anayejipenda anapotoka kwenda iwe ofisini,kanisani kwenye sherehe au hata sokoni lazima atakuwa na pochi yake mkononi.

Ubebaji wa vitu ndani ya pochi ndiyo unapoleta maana kwa mwanamke ingawa sambamba na umuhimu wake huo pia huongeza umaridadi wa mbebaji endapo atakwenda sambamba na mtindo kwa mvaaji.
Kama ilivyo kwa mavazi,pochi nazo zipo za aina mbali mbali,na aina zote zinabebwa kulingana na mahitaji ya muhusika muhusika mwenyewe.


Mfano pochi inayobebwa na mtu anayeenda harusini au kwenye mitoko ya jioni maarufu kama 'Purse au clutch'  haifai kubebwa na mtu anayeenda ofisini halika dhalika pochi inayobebwa na mtu anayeenda kwenye sherehe ya jioni au sherehe yoyote haipendezi kuendea ofisini au kutembelea mchana.

Kwa kawaida pochi ya harusini huwa ndogo na inayonga'a tofauti na pochi ya kuendea kazini huwa kubwa au ya saizi ya kati na mara nyingi inakuwa na rangi moja au mbili.
Pochi ya kubeba kwenye sherehe hususani sherehe za jioni halikadhalika huwa ndogo na inayofanana na moja ya vazi ulilofaa iwe viatu, kofia ama mkanda.

Aina za pochi zinaleta maana zaidi kwa mbebaji kutokana na aina ya nguo uliyovaa na eneo unaloenda mfano pochi ya ofisini inapendeza ikiwa ya wastani ambayo inauwezo wa kubeba wallet ndogo ya pesa, diary, kipochi kidogo cha vipodozi nk.
Wengi hupenda kubeba pochi lakini sio wote wanaozingatia matumizi ya pochi na umuhimu wake katika mitindo.
Zingatia na jali kuwa maridadi na nadhifu wakati wote.

3 comments:

  1. THANX Mamy. ur blog loking very nice

    ReplyDelete
  2. Hongera sana ndauka pro.

    ReplyDelete
  3. heheheheeee we Rachel nipe ramani fasta wapi hizo pochi? ramani plzzz

    ReplyDelete