Wednesday, May 30, 2012

BARNABA ALITAKA KUTOROKA UKUMBINI

                                              Barnaba Elias
Barnaba afunguka ndani ya bongo beats ya star tv .
Msindi wa tuzo za kill music awards Barnaba Elias msanii kutoka THT ambaye pia ni baba wa mtoto mmoja (stephen) alitaka kutoka kimya bila kuaga mtu yoyote (kutoroka) siku ya kilimanjaro music award baada ya kuona tuzo karibia zote zimetolewa na yeye akiwa bado hajapa hata moja wakati huo ikiwa imebakia nafasi moja tu ya mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka. Barnaba alivunja mpango wake huo akiwa nyuma ya jukwaa tayari kwa kuondoka baada ya kusikia yeye ndiyo mshindi wa tuzo hiyo moja iliyobakia ya mwanamziki bora wa kiume wa mwaka.
Mbali na hapo Barnaba ametangaza kupanda dau kwa waandaaji wa matamasha kutokana na dhamani aliyonayo hivi sasa.



No comments:

Post a Comment