WAANDAAJI wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Kigamboni City 2012
wameomba wasichana wenye sifa zinazostahili kujitokeza kushiriki katika
shindano hilo.
Mratibu wa Redd’s Miss Kigamboni City, Somoe Ng’itu, alisema jijini
Dar es Salaam jana kwamba tayari baadhi ya warembo wanaotarajiwa
kushiriki shindano hilo wameanza mazoezi, lakini bado wanakaribisha
wasichana wengine.
“Ndiyo kwanza tumeanza mazoezi juzi katika ukumbi wa Break Point
katikati ya jiji la Dar es Salaam, lakini milango iko wazi kwa wasichana
wengine kujitokeza ili kuleta ushindani kwenye shindano letu,” alisema
Somoe.
Aliongeza kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vema, ambalo
litakalofanyika Juni 15 kwenye Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni yanakwenda
vema. Warembo hao wanafanya mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa
mshindi ya shindano la Kanda ya Temeke 2003.
Somoe, aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi kuwa ni pamoja na
Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar,
Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili na Doreen
Kweka.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano
hilo kuwa ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji
chake cha Redd’s Origal, Dodoma Wine na NSSF.
No comments:
Post a Comment