KUNDI la muziki wa taarabu la Manowari Modern Taarab linatarajia 
kufanya uzinduzi wa kundi na albamu yao kwenye Ukumbi wa Hoteli ya 
Traventine, Magomeni jijini Dar es Salaam, Jumatano ya Mei 30 .
Msemaji wa kundi hilo, Maliki Kizo, alisema jana kwamba wamejipanga 
vema kuhakikisha uzinduzi huo unafana kwa kuimba nyimbo zao mpya 
walizorekodi katika ubora wa hali ya juu.
Alisema, kundi hilo ambalo lilianzishwa mwaka 2008 likipiga zaidi 
taarabu ya kiasili, limejipanga kuhakikisha linaleta mapinduzi na kuwapa
 raha ya kutosha mashabiki wa muziki huo.
Alizitaja nyimbo zilizopo katika albamu yao ya kwanza iitwayo ‘Sogea 
Nikwambie’ ni pamoja na ‘Sogea Nikwambie’ iliyobeba jina la albamu, 
‘Sigara Kali’, ‘Shani’, ‘Najuta Kukufahamu’, ‘Kawaambie Wenzako’, ‘Vipi 
penzi liwe Uadui’, ‘Mwanzo wa Yote’ na ‘Hawajui Twapendana’.
Wasanii wanaounda kundi hilo ni pamoja na aliyewahi kuwa nyota wa 
muziki wa Kizazi kipya, Ally Com, Abdi Omari, Samiu Issa, Sophia Saleh, 
Shamim Hassan, Sauda Adam, Christina Matosi, Amina Salim na Sina Hassan.
 Kundi la muziki wa dansi la Chuchu Sound linatarajiwa kusindikiza 
uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment