SHINDANO la kumsaka Redd’s Miss Dar Intercollege 2012
linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Sunciro, ulipo Sinza Shekilango
jijini Dar es Salaam Juni 8 mwaka huu.
Mratibu wa Shindano hilo, Dina Ismail, alisema jijini Dar es Salaam
jana kwamba warembo watakaoshiriki shindano hilo wanaendelea na mazoezi
kwenye hoteli ya Lamada jijini chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface,
huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.
Alisema, hadi sasa warembo 12 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi
wa Habari (DSJ), na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa
Fedha (IFM), wameisharipoti kambini.
Dina, aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy
Maganga, Saada Seleman, Neema
Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus,
Jane Augustino, Theresia Isaya na Natasha Deo. Taji la kitongoji hicho
linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameziomba kampuni mbalimbali
kujitokeza kudhamini shindano hilo, ambalo linatarajiwa kuwa la aina
yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya
juu.
“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano
letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), kupitia bia ya Redd’s Original, Lamada Hotel, Ndege Insurance,
Dodoma Wine na Clouds Fm.
No comments:
Post a Comment