BIA ya Kilimanjaro Premium Lager imezindua Kampeni kubwa ijulikanayo
kama 100% TZ Flava yenye kaulimbiu ya ‘Sherehekea Kilicho Chetu’
itakayoendeshwa kwa miezi sita mfululizo.
Kampeni hiyo ya aina yake inayolenga kuwahamasisha Watanzania kujivunia mambo mbalimbali ya Kitanzania kama vile muziki, lugha na michezo, ilizinduliwa katika ukumbi
wa Nyumbani Lounge juzi.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alizindua kampeni hiyo akisema kwamba itaendelea kwa miezi sita kuanzia sasa, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni
ya Kili Jivunie u-Tanzania iliyofanyika mwaka jana kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.
Alisema shughuli ya kwanza ilikuwa kuzindua alama ya kampeni hiyo, 100% TZ Flava- tusherehekee kilicho chetu na nyingine zitafuatia ndani ya miezi sita ambapo kampeni hiyo
itawafikia Watanzania nchi nzima.
“Kampeni hii imeandaliwa kumpa mteja raha, lakini lazima iache ujumbe, ambao ni Sherehekea kilicho chetu,”alisema Kavishe.
Kipa wa Yanga, Shaaban Kado na winga wa Simba Salum Machaku walipamba vyema onesho hilo la uzinduzi ambapo walishiriki kwa pamoja na wasanii wa kundi la THT na waigizaji nyota wa filamu Tanzania, Aunt Ezekiel na Jacob Steven ‘JB’, nyota wa muziki wa Hip hop, Joseph
Haule ‘Profesa Jay’ na mwimbaji wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Janet Isinike.
Kwa mujibu wa Kavishe kampeni hiyo imetumia picha za Simba na Yanga, klabu ambazo zinadhaminiwa na bia hiyo.
Katika kampeni hiyo pia wametumia lugha za mtaani, ambazo Kavishe alisema ni fahari ya Tanzania kwa mfano piga tarumbeta, neno linalowakilisha kunywa bia kwa kutumia chupa moja kwa moja na kula bata, yaani kula raha.

CHANZO CHA HABARI:http://www.habarileo.co.tz/michezo/?n=30566&cat=michezo
No comments:
Post a Comment