MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), leo anatarajia 
kuchangisha sh milioni 220 katika tamasha la nyimbo za injili 
litakalohitimisha mpango wa Wezesha Upendo Redio kwa ajili ya ununuzi wa
 vifaa vitakavyosaidia kuwepo kwa usikivu bora wa vipindi.
Katika tamasha hilo litahudhuriwa na waimbaji kama Sara K kutoka Kenya Faraja Ntaboba wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), wengine kutoka nyumbani ni Jackson Bent kutoka Arusha, Jennifer Mgendi na kwaya ya KKKT kutoka makanisa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani (KKKT), Mchungaji Richard Jackson, ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi, alisema tamasha hilo litafanyika leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Richard alisema mpango wa kuwezesha redio hiyo ulizinduliwa Februari mwaka huu kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za uinjilishaji na kuielimisha jamii kupitia vipindi vyake.
Aliongeza kuwa, mpango huo umetoa changamoto hususani katika kipindi hiki ambacho vyombo vya habari vya kielekroniki vinapaswa kutoka kwenye mfumo wa utangazaji wa analogi kwenda digitali.
“Mabadiliko haya ni lazima kwa mujibu wa sheria za nchi kuyafanya, sisi kama Upendo Redio si madogo… ni gharama hivyo licha ya kuhitimisha mpango huu tutaendelea na mkakati wa kutafuta pesa zaidi ili kuweza kuboresha kituo chetu.
“Redio Upendo ilianzishwa mwaka 2004 ambapo kwa sasa inasikika katika mikoa saba,” alisema mchungaji huyo na kuongeza kwamba, tamasha hilo litapambwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka nje na ndani ya nchi, wakiwemo Sarah kutoka Kenya na Faraja Ntaboba kutoka DR Congo.
CHANZO GAZETI LA HABARI LEO LA JUMAPILI YA LEO

No comments:
Post a Comment