Petr Cech ameamua atasalia katika klabu ya Chelsea, angalau kwa miaka mine ijayo, kufuatia kutia saini mkataba wa muda huo.
Kipa huyo ambaye amehudumu Chelsea kwa muda mrefu, ameichezea timu ya The Blues katika mechi 369, tangu alipojiunga na klabu mwaka 2004.
                     
Ataichezea Chelsea kwa miaka minne ijayo
Sasa atakuwa Stamford Bridge hadi mwaka 2016.
"Ninafurahi mno kuwa ni sehemu ya klabu hii 
maarufu kwa kipindi cha miaka mine zaidi," alielezea mchezaji huyo 
mwenye umri wa miaka 30.
"Ninatumaini miaka hiyo minne ijayo itakuwa ni sawa na miaka minane ambayo nimekuwa nikikichezea klabu."
Cech, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa umalizike mwaka ujao, ni mchezaji muhimu kwa Chelsea
Baadhi ya mafanikio ya Chelsea Cech akiwa ni 
kipa ni pamoja na kupata ubingwa wa ligi kuu ya Premier mara tatu, 
ubingwa wa Kombe la FA mara nne, ushindi wa Kombe la Carling mara mbili,
 na hivi majuzi, ubingwa wa UEFA wa klabu bingwa barani Ulaya kwa mara 
ya kwanza.
Cech pia alitangazwa kama mchezaji bora zaidi wa Chelsea mwaka jana, 2010/11.
"Chelsea inatambua kikamilifu mchango muhimu 
kutoka kwa Petr wakati huu wa klabu kupata ufanisi wake mkubwa zaidi 
katika historia yake," alielezea mkurugenzi mkuu wa Chelsea, Ron 
Gourlay.
Kipa msaidizi wa Cech, Thibaut Courtois kutoka 
Ubelgiji, huenda akaachiwa mechi zaidi za ligi kuu ya Premier ili 
kujinoa zaidi, baada ya kuonyesha uhodari wake akiwa mchezaji wa mkopo 
katika klabu ya Uhispania ya Atletico Madrid, ijapokuwa kijana huyo wa 
miaka 20 huenda akaazimwa kwa timu nyingine kwa muda mfupi.
Courtois alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya 
Racing Genk, mwezi Julai mwaka jana, na kwa kuelekea Uhispania na 
kutofungwa, aliiwezesha klabu ya Atletico Madrid kuibuka mabingwa wa 
klabu ya Europa mapema 
No comments:
Post a Comment