Monday, May 14, 2012

USAFI/UREMBO WA NGOZI




 

 NGOZI ni kiungo kilichochukuwa nafasi kubwa katika mwili wa binadamu. Kutokana ukweli huu kiungo hiki kinahitaji na kustahili uangalizi wa kila siku.
 tunaangalia utunzaji wa ngozi ya uso wakati wa usiku. 
Kwa kuwa utaratibu wa utunzaji wa ngozi wa uso wakati wa mchana unalenga kuamsha ngozi na kuiandaa kwa ajili ya shughuli za mchana, kwa wakati wa usiku, unalenga  kuipa ngozi nafasi ya kupumzika.
Wataalamu wa mambo ya urembo wanashauri , usafi wa ngozi kabla ya kupanda kitandani. 
Hivyo katika kuhakikisha usafi huo, kuna baadhi ya vipodozi muhimu vinavyohusika kwa shughuli hiyo, vipodozi hivyo ni kama vifuatavyo;
 ‘Make up remover’- Hivi ni vipodozi  maalum vinavyotumika kuondoa vipodozi vingine katika ngozi.  Hivyo katika utaratibu wa kusafisha ngozi, hii ni hatua ya kwanza kabisa. 
Mara nyingi ‘remover’ hizi hutofautina kulingana na aina ya kipodozi unachotaka kuondoa. Kwa mfano ikiwa unahitaji kuondoa wanja ama rangi ya mdomo, tumia mafuta ya  maji kama vile mafuta ya nazi n.k
Kwa aina nyingine za vipodozi kwa mfano poda, foundation na shedo za macho unaweza kutumia tona ama ‘cleanser’.
Hakikisha unatumia pamba kwa kuchovya kwenye ‘remover’ hizo na kisha kupangusa ngozi yako ukilenga kuondoa vipodozi hivyo. 
Hakikisha hausugui ngozi kwa nguvu ili kuepuka kusababisha michubuko katika ngozi yako.
Baada ya kuhakikisha uchafu  na vipodozi vyote vimetoka katika ngozi, pakaa krimu ya usiku. Krimu hii nayo imegawanyika katika sehemu mbili. Kuna ile ya kupaka usoni kwa ujumla na nyingine ni maalum kwa kupaka chini ya macho.
Vipodozi vya mchana ni maalum kwa kuilinda ngozi katika mazingira ya mchana na hivi vya usiku vinalenga kuilinda ngozi na kuifanya iweze kumpumzika na kupumua vyema na hivyo kuzidi kujijenga kiafya zaidi.
Wataalamu wanashauri, vipodozi vya mchana kutumika mchana na vya usiku vitumiwe usiku. 
Ikiwa utatumia vipodozi vya usiku wakati wa  mchana, ngozi yako itakuwa na mafuta  na hivyo kuiweka katika hatari ya kuzalisha chunusi.
 
imeandaliwa na rachael ndauka
rndauka@gmail.com


2 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. naomba unifahamishe rosheni ya clear essence inatumika kwa mtu anayetaka kuwaje. mfano kuwa mweupe au kawaida, naomba unifahamishe ndungu yangu.

    kutoka Bukoba

    ReplyDelete