TAREHE YA MISS NYAMAGANA YABADILISHWA SASA KUFANYIKA JUNE 01, 2012

Warembo 20 kutoka wilaya ya Nyamagana Mwanza.
Stoppers Entertainment inakuletea Miss Nyamagana 2012 Mwanza. Warembo wenye Haiba, Tabasamu, Minato na Catwalk ya uhakika. 
Shindano litafanyika ijumaa ya tarehe 01 june 2012, saa 2 usiku katika ukumbi wa Gold crest Mwanza.
Kwa kiingilio cha Tsh 20,000/- Mashabiki watashuhudia shindano hilo.
Burudani ni pamoja Mwanamuziki Linah, mara baada ya ziara yake ya nchini Marekani, show yake ya kwanza, itakua jijini Mwanza, Mwingine ni Ditto kutoka THT, pamoja na mwanamuziki Hafsa Kazinja aliyetamba na kibao chake cha Pressure akimshirikisha Banana Zorro.
MC au Mshehereshaji mkuu katika shindano hilo ni muigizaji maarufu katika tasnia ya uchekeshaji namzungumzia Mpoki.
Shindano la Miss Nyamagana 2012, linadhaminiwa na Furniture House Mwanza, Redds Original, Pepsi, Star TV, Nyota Rays LTD, Far end Travel, Mukesh Vunja bei, Whitney Fashion. Perfect Salon, Victoria Institute of Hotel management, Photo Spot, The Big Top Ten.Blogspot.com na gsengo.blogspot.com