MABINGWA wa mipasho, Jahazi Modern leo wanatarajiwa kukonga 
nyoyo za mashabiki wao wa Mbagala pale watakapotumbuiza kwenye ukumbi wa
 Dar Live, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, 
Mkurugenzi Mkuu wa Jahazi Modern, Mzee Yussuf ‘Mfalme’ alisema kuwa, 
onesho hilo la leo limepewa jina la ‘Usiku wa Vidole Juu’.
Yussuf alisema kuwa katika onesho hilo, kikosi chake kinachokusanya 
nyota wengi wenye vipaji vya hali ya juu, kimepanga kuacha simulizi kwa 
kurindimisha burudani ya kukata na shoka.
“Nawaomba mashabiki pamoja na wapenzi wote wa mipasho, katika 
kitongoji cha Mbagala na Wilaya nzima ya Temeke, kufika kwa wingi katika
 onesho hilo ili kufaidi mambo matamu tuliyowaandalia,” alisema Yussuf.
  Yussuf, alitaja baadhi ya mambo waliyopanga kuwaloga nayo mashabiki na
 wapenzi watakaohudhuria onesho hilo, kuwa ni pamoja na nyimbo mpya na 
vionjo vya kukata na shoka walivyovibuni hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment