Monday, June 4, 2012

Noti tupu Fainali za Euro 2012


ZURICH, Uswisi
FAINALI za Euro 2012 zitaanza mwishoni mwa wiki hii kwa mapambano ya Kundi A kati ya Poland na Ugiriki kwenye mji wa Warsaw wakati Russia itapambana na Jamhuri ya Czech kenye mji wa Wroclaw.

Lakini mbali ya mechi hizo, Shirikisho la Soka Ulaya, Uefa, limetangaza 'mihela' kwa timu zinazoshiriki fainali hizo. Jumla ya fedha ambazo timu zitavuna zinafikia euro 200mil.

Uefa imesema jumla ya shughuli zote ni fedha hizo (euro 200) ikiwa ni zaidi ya euro 184 milioni kwa zawadi za zilizokuwa Fainali za Euro 2008.

Mchakato uko hivi: Kila timu itakayoshiriki itapata euro8 milioni na timu itakayofanya vizuri (kushinda mechi nyingi makundi, nidhamu nzuri) itapata bonasi ya euro 500,000.

Mbali na bonasi hiyo, timu itakayoshinda kwa kila mchezo, itapata euro1 milioni wakati timu itakayoshika nafasi ya tatu katika kila kundi, itaondoka pia na fedha hiyo euro 1mil.

Timu zitakazoingia robo fainali, kila mmoja atalamba euro2milioni na nusu fainali kila timu itapata euro 3 milioni huku mshindi wa pili akiondoka na euro 4.5 milioni. Bingwa ataondoka na kitita cha euro 7.5 milioni.

(NB: 1 euro = Tsh2,000)

No comments:

Post a Comment