BONDIA wa Urusi, Vitaly Shemetov maarufu kama ‘Siberian Tiger’
ameingia mitini yeye na kocha wake kuja nchini kupambana na mkongwe,
Rashid Matumla ‘Snake Man’.
Shemetov na kocha wake, walitumiwa tiketi za ndege ya shirika la
Kirusi la Aeroflot, ili kuja nchini kwa ajili ya pambano hilo
litakalorindima Juni 24 mjini Moshi, wakati wa Mbio za Mount
Kilimanjaro.
Kwa mujibu Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF),
Onesmo Ngowi, hii ni mara ya kwanza kwa pambano la kimataifa
lilioandaliwa kwa fedha nyingi, kutofanyika baada ya bondia huyo kuingia
mitini kwa madai ya woga.
Ngowi alisema, Matumla ana rekodi ambayo hadi sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.
“Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na Kati,
Bara la Afrika, mabara na dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani
(WBU),” alisema Ngowi na kuongeza; akiwa chini ya DJB Promotions,
bondia huyo ambaye kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalumu ya Dar
es Salaam, alionyesha alionesha kiwango cha hali ya juu.
No comments:
Post a Comment