Bodi ya Taifa ya
Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, katika kutekelezaa mpango mkakati wake wa
kuimarlisha na kuboresha zaidi mashindano hayo, imegawanya mikoa yote ya Tanzania
na Vyuo Vikuu katika kanda maalumu za mashindano hayo.
Kwa lengo la
kuimalisha utekelezaji wa malengo ya mashindano na usimamizi , Kuanzia mwaka
huu kutakuwa na jumla ya kanda 14 za mashindano ya Miss Utalii Tanzania ,
zikiwemo saba (7) za kawaida na saba (7) kanda maalumu za Miss Utalii vyuo Vikuu.
Hatua inalenga pia kufikisha mashindano ya Miss Utalii Tanzania hatika Ngazi za
chini zaidi , mijini na vijijini, ambapo kwa kuanzia mashindano haya sasa
yataanzia katika Ngazi za kata, Majimbo ,Wilaya,mikoa, kanda, taifa na hatimaye
Dunia, hiku mpango mkakati ni kuanza kufanyika katika mgazi za vijiji ifikapo
mwaka 2014. Huu ni mpango wa lazima kwetu kwa mujibu wa kanuni na taratibu za
mashindano haya, ambayo pamoja na malengo mengine yanalenga pia kuelimisha na
kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa sekta ya Utalii kiuchumi na kijamii,hivyo
kuwa fulsa pekee ya kufanyika kwa mashindano haya katika Ngazi za vijiji
lufikia mwaka huo 2014.
Mgawanyo wa kanda hizo
na mikoa yake katika mabano ni:
A: KANDA ZA KAWAIDA
NI:
1. Miss Utalii Tanzania –Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara,
Zanzibar)
2. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Magharibi (Simiyu, Shinyanga na Mara)
3. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Ziwa (Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma)
4. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro na Arusha)
5. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kati (Tabora, Dodoma, Singida na Morogoro)
6. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kusini
Nyanda za Juu (Mbeya, Rukwa na Katavi)
7. Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kusini (Ruvuma, Iringa na Njombe)
B: KANDA MAALUM ZA
VYUO VIKUU NI:
1. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kati
(Dodoma, Kigoma,
Tabora, Singida)
2. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini (Iringa, Ruvuma, Njombe)
3. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Pwani (Dar es Salaam, Zanzibar , Lindi na Mtwara)
4. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu- Kanda ya Magharibi (Mwanza, Geita, Kagera,
Mara, Simiyu, Shinyanga na Singida)
5. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini Nyanda za Juu (Mbeya, Rukwa, Katavi)
6. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kaskazini ( Arusha,Kilimanjaro,Manyara)
7. Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Mashariki (Morogoro, Mtwara
na Lindi)
Mgawanyo huu wa kanda
umezingatia , maeneo ya kijografia, mwingiliano wa tamaduni, uwepo wa vivutio
vya Utalii katika kila kanda, urahisi wa kutangaza Utalii na kuhamasisha Utalii
wa ndani,pia kutoa fulsa kwa mabinti wengi zaidi kushiriki mashindano haya
katika Ngazi zote.
Aidha mfumo huu,
utasaidia kuwachuja washiriki katika Ngazi za kanda, hivyo kuwa na washiriki
wenye viwango na ushindani unaokibalika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za
mashindano haya na mengine yahusuyo kitaifa na kimataifa.
Kwa mwaka huu, kanda
ya ziwa ndiyo itakayo kuwa ya kwanza kufanya Fainali zake za Miss Utalii Kanda
ya Ziwa 2012 na kushirikisha jumla ya warembo 15 kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera,
Geita na Kigoma. Shindano hilo linalo andaliwa na Fania Hassani ambaye ni
Mkurugenzi wa Miss tourism Tanzania Organisation kanda ya Ziwa na Fania Beauty
Saloon ya limepangwa kufanyika Juni 30, 2012 katika ukumbi wa Monarch Hotel Mwanza
na kudhaminiwa na Gold Masters, Monarch Hotel, Garrett Security Items na Solar
Power MSP – H na magazeti ya Gazeti la Jambo Leo, KIU Investment.
(picha zilizo
ambatanishwa na Taarifa hii ni za washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012- Kanda
ya Ziwa, wakiwa wamepozi katika hoteli ya Monarch ambako kambi ya Mazoezi
inaendelea, tayari kwa Fainali itakayo fanyika hotelini hapo 30-6-2012.
Asante,
By Mr. George Ntevi - Katibu wa Bodi ya Taifa ya Mashindano ya
Miss Utalii Tanzania .
No comments:
Post a Comment