Miss Kigamboni 2012, Edda Sylvester (katikati)
akiwa na mshindi wa pili Agnes Goodluck (kushoto) na mshindi wa tatu
Elizabeth Boniphace mara baada ya kutangwazwa washindi.
Edda Silyvester, 21, ambaye ni mwanafunzi wa shahada
ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani alitwaa
taji la Miss Kigamboni katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa
Navy Beach usiku wa kuamkia jana, na kuingia hatua ya Kanda akiongoza
wasichana wengine wanne.
Jaji mkuu wa shindano hilo, Benny Kisaka,
alitangaza kuwa badala ya warembo watatu, watachukua warembo washindi
watano wa kwanza miongoni mwa washiriki tisa kuingia shindano la Kanda
ya Temeke baadaye mwaka huu.
Kutokana na ushindi huo Edda alizawadiwa
Sh.500,000 taslimu na mgeni rasmi katika shindano hilo, diwani wa Kata
ya Kigamboni, Dotto Msawa.Nafasi ya pili katika shindano hilo
lililopambwa na burudani safi kutoka bendi ya FM Academia 'Wazee wa
Ngwasuma' ilichukuliwa na Agnes Goodluck ambaye alipata zawadi ya
Sh.350,000.
Elizabeth Boniface alichaguliwa kuwa
mshindi wa tatu na kupata zawadi ya Sh.300,000. Esther Albert na Khadija
Kombo walishika nafasi za nne na tano na kila mmoja alipata zawadi ya
Sh.200,000.
Warembo wengine walioshiriki shindano hilo
walikuwa ni Sophia Martin, Rosemary Peter, Doreen Kweka na Linnah David
waliopewa kifuta jasho cha Sh.150,000 kila mmoja.
Wakati huo huo, Matlda Martine alitwaa taji la Miss Dar City Centre katika shindano lingine lililofanyika jijini juzi usiku pia.
No comments:
Post a Comment