HARAKATI za kupata wawakilishi wa shindano la Miss East Africa
2012 zimeendelea, ambapo Akuot Philip Suzan (20) ametwaa taji la nchi ya
Sudan Kusini.
Mkurugenzi wa Rena Events inayoratibu shindano la Miss East Africa, Rena Callist alisema jana kwamba, mrembo huyo mwenye urefu wa futi 6.1 anatarajiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Makelele kilichopo nchini Uganda baadaye mwaka huu.
Alisema, mrembo huyo ataungana na washiriki wengine kutoka nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki kushiriki fainali za shindano hilo ambalo limepangwa kufanyika Septemba 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Tayari warembo kutoka nchi nne wameshapatikana wakiwamo Rahwa Afeworki (22), wa Eritrea, Lula Teklehaimanot (19) kutoka Ethiopia na Ayisha Nagudi (23,) ambaye ni mwakilishi wa Uganda.
Nchi zitakazochuana katika shindano hilo ni pamoja na Tanzania, Sudan Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36666

No comments:
Post a Comment